JUSTIN BIEBER ABATIZWA BAFUNI KWA RAFIKI YAKE

Justin BieberMchungaji Carl Lentz Amemsaidia Mwanamuziki Justin Bieber kufuta dhambi zake zote na kuzaliwa mara ya Pili kwa kubatizwa na kujiunga rasmi na imani ya kikristo. Ubatizo ambao umefanyika bafuni kwa rafiki yake.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amechukua uamuzi huo ikiwa ni wiki chache kupita tangu zivuje video zinazomuonesha akifanya utani wa kiubaguzi wa rangi alipokuwa na umri wa miaka 15.

Mchungaji Carl Lentz aliyembatiza Justin Bieber ameiambia TMZ kuwa alitumia wiki moja kufanya mafundisho ya kina ya biblia na Justin Bieber mwezi uliopita kabla video za kibaguzi hazijavuja, na ilikuwa ni siku chache kabla hajafuatwa na mtu aliyetaka ampe dola milioni moja ili asizitoe video hizo.

Ameeleza kuwa Justin Bieber amekuwa akisoma Biblia mara kwa mara na kuhudhuria mafundisho ya dini lakini alikuwa hajapata kanisa ambalo angeweza kubatizwa bila kuingiliwa hivyo aliamua kuchagua kufanya ubatizo huo ndani ya bafu la rafiki yake(ndani ya bathtub) ili kuweka usiri.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s