FRENCH MONTANA NA KHLOE HAKUNA SIRI TENA, WAWAKIVUTIO KWENYE TUZO ZA MTV MAMA

French Montana & Khloe Kardashian

 Rapa mwenye asili ya Morocco French Montana na mrembo daraja la kwanza Khloe Kardashian usiku wa jana walikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waliohudhuria sherehe za utoaji wa Tuzo za MTV MAMA zilizofanyika mjini Durban nchini Afrika Kusini hasa kutokana na mastaa hao  kuripotiwa na vyombo vingi vya habari  kuwa kwenye  mahusiano ya siri kimapenzi licha ya kukanusha na kudai kuwa ni marafiki tu.

Awali Khloe anayetokea katika familia ya The Kardashian alikuwa ni mke halali wa mcheza kikapu Lamar Odom kabla ya wawili hao kuamua kupigana chini mwishoni mwa mwaka jana, licha ya zilipendwa wa mwanadada huyo kuwa mbishi kwa kutokubali matokeo.

Hitmaker huyo wa Pop That alikuwa miongoni mwa wasanii wa kimataifa walioalikwa kutoa burudani kwenye jukwaa la MTV MAMA sambamba na wakali wengine akiwemo Trey Songz, Miguel na Marlon Wayans.. 

French & KardashianFrench Montana na Khloe

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s