BREAKING NEWZZZ : MZEE SMALL AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 59

Mzee Small

Pichani ni Mzee Small enzi za uhai wake na Mkewe Bi Fatuma Saidi

Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mwigizaji maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini Tanzania, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.  Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhumbili.

Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma Saidi, aliithibitishia blog ya Father Kidevu , kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.

Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na umauti baada ya hali yake kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza Muhimbili ambako alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku alirudi nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na ilipotimu saa tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.

“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni maneno machache yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe.  Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.

Blog ya Larrybway91 inatoa salamu za pole kwa familia na wafiwa wote waliofikwa na msiba huyo. 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s