MBEYA CITY YAPATA MKATABA MNONO WA MILIONI 360 KUTOKA KWA KAMPUNI YA BINSLUM

Mbeya CityTimu ya mpira wa miguu ya jijini  Mbeya maalufu kama Mbeya City FC (WABISHI)  wameingia mkataba wa miaka 2 wa udhamini wa timu hiyo ya ligi kuu Tanzania na kampuni ya Binslum Tyre Company Ltd.

Binslum Tyre Company Ltd inayomilikiwa na Mohamed Bimnslum imeingia mkataba huo kwa gharama za Tsh. 360 Milioni kwa miaka miwili kuanzia msimu huu.

Mohamed Bimnslum ameamua kumwaga pesa zake katika klabu hiyo ya jiji la Mbeya ambayo ilipanda ligi kuu mwaka jana na kuleta upinzani mkubwa baada ya kusumbuana na uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo alikuwa anaidhamini toka mwanzo.

“Kwa kutambua hilo tumeamua kuidhamini timu ya mpira wa miguu ya Mbeya City ya jijini hapa kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia tatu na sitini (360,000,000)” Amesema Mkurugenzi wa Binslum Tyre Company Ltd, Ndugu Mohamed Binslum alipokuwa kwenye sherehe ya makabidhiano na wamiriki wa timu hiyo jijini Mbeya.

“Udhamini huu ambao ni wa kwanza kwa Kampuni yetu kudhamini timu za nje ya Dar Es Salaam unalenga kuiimarisha timu ya Mbeya City ili kufanya vizuri zaidi katika ligi kuu kwa misimu ijayo, pia kuendeleza mpira wa miguu hapa jijini na Tanzania Kwa ujumla” Ameongezea Binslum.  

Kwa mkataba huo sasa Mbeya City  msimu huu itakuwa inatangaza betri za RB katika jezi kwa mbele kama ilivyo sheria kuwa mdhamini mkubwa wa timu logo au bidhaa yake inakuwa mbele ya jezi.

Mbeya City sasa itakuwa na mafanikio makubwa baada ya kupata udhamini huo huku ikiwa chini ya uangalizi wa manispaa ya jiji la Mbeya.

“Pia ni njia mojawapo ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu makampuni kujikita katika kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini” Amemalizia Binslum.

-PesaTimes.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s