BILIONEA OPRAH WINFREY AZIDIWA KETE NA MKURUGENZI WA MICROSOFT KATIKA UNUNUZI WA TIMU YA LOS ANGELS CLIPPERS

Steve Ballmer

Bilionea mwenye asili ya Afrika kutoka nchini Marekani ‘Oprah Winfrey’ amekosa nafasi ya kuinunua timu ya mpira wa kikapu ya Los Angels Clippers kufuatia kiwango cha pesa alichoweka kuzidiwa kwa dola milioni 2  na kiwango kilichotolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Microsoft Steve Ballmer.

Awali Oprah Winfrey, Antony Ressler, Steve Ballmer pamoja na mchezaji wa zamani wa Lakers Magic Johnson ndio waliotajwa kuwania nafasi ya kutaka kuinunua timu hiyo licha ya hapo baadae mambo kugeuka.

L.A ClipersOprah Winfrey, Antony Ressler, Magic Johnson na Steve Ballmer

Oprah mwenye umri wa miaka 60 ambaye kwa sasa anarekodi kipindi  kipya amesema kuwa ameshangazwa na hatua ya kuwekewa vikwazo yeye kama mwanamke kununua timu hiyo ya mpira wa kikapu na kufikiri sana juu ya suala hil.

Alinukuliwa akisema kwamba kiwango chake cha mwisho ni dola bilioni 2 ambapo amesema tangu aweke hadharani kukasirishwwa kwake na kitendo hicho amejisikia nafuu kiasi.

Timu ya Los Angels Clippers yenye wachezaji nyota kama vile Blake Griffin na Chris Paul ilikumbwa mgogoro majuma kadhaa yaliyopita baada ya mmiliki wake ‘Donald Sterling’ kumtolea matamshi ya kibaguzi mpenzi wake, hali  iliyopelekea afungiwe na chama cha NBA  kutojuhusisha kwa namna yoyote na timu hiyo kabla ya kushauriwa kuibiga bei.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s