RIPOTA ALIYETAKA KUTOA ROHO YA BRAD PITT AHUKUMIA KIFUNGO CHA MIAKA 3

Brangeline

Brangelina

Mwanaume mmoja ambaye ni ripota kutoka nchini  Ukreini ‘Vitalii Sediuk’ amehukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu, siku ishirini za kufanya kazi za jamii  na kutakiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake baada ya kumshambulia staa nyota wa filamu kutoka Hollywood ‘Brad Pitty’ hadi kumvunjia miwani yake katika uzinduzi wa filamu ya Maleficent aliyocheza mkewe bibie Angelina Jolie kwenye ukumbi wa El Captain Theatre

Ripota huyo anakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo kufanya uhalifu kinyume cha sheria huku Jaji wa mahakama iliyotoa hukumu hiyo pia imemwagiza kukaa mbali na matukio yanayohusisha zulia jekundu, uzinduzi wa filamu pamoja na matukio ya burudani.

Vitalii Sediuk

Vitalii Sediuk

Sediuk aliachiwa kutoka kizuizini baada ya kufika mahakamani lakini anatakiwa kufika tena mahakamani hapo julai 8 mwaka huu kuangalia utendaji wake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Sediuk kuwafanyia vituko kwa mastaa, kwani hata Mei 23 mwaka 2012 aliwahi kuchapwa kofi na muigizaji Will Smith baada ya kumkumbatia na kumpiga busu kitendo kilichoonekana kumchefua staa huyo wa filamu za Bad Boys. Tazama ilivyokuwa hapo chini

Hii ilikuwa mwaka 2012 wakati Sediuk alipojaribu kumchumu Will Smith na kisha kuambulia kofi

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s