BREAKING NEWZZ : GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI MKOANI MOROGORO

George Tyson

George Tyson

Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania  mwenye asili ya Kenya, George Tyson amefariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari   wakati wakitokea kwenye hafla ya kuadhimisha miaka miwili ya kipindi cha luninga cha The Mboni Show mkoani Dodoma kufuatia gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Noah kupasuka matairi   na kuanguka eneo la Gairo mkoani Morogoro majira ya saa moja jioni.

Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam

Awali Tyson aliwahi kuwa mume wa muigizaji nyota wa kike wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ aliyeza nae mtoto mmoja wa kike anayeitwa Sonia.

Atakumbukwa kwa ucheshi, ukarimu na busara zake, Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi Ameen.

The Mboni ShowPichani ni mtangazaji wa kipindi cha The Mboni Show, Mboni Masimba akikabidhi madawati kwa mkuu wa shule ya msingi ya Chalula iliyopo Chinolwa, Chamwino mkoani Dodoma wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya kipindi hicho ikiwa ni masaa machache kabla ya kutokea kwa ajali iliyochukua uhai wa Tyson.

Monalisa na TysonGeorge Tyson enzi za uhai wake akinyweshwa kinywaji na mzazi mwenzake Monalisa wakati wa sherehe ya kipaimara cha mtoto wao Sonia(Pichani Kulia)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s