RAPA T.I ACHAPANA MAKONDE NA BONDIA FLOYD MAYWHEATHER, WIVU WATAJWA

Floyd Mayweather Jr. Hosts Party At MGM's Studio 54

T.I na Maywheather enzi hizo

Rapa maarufu anayetokea katika mji wa Atlanta, Georgia   ‘Clifford Joseph Harris, Jr’ AKA T.I amejikuta akiingia kwenye ugomvi  na aliyekuwa rafiki yake bondia milionea ‘Floyd Money Maywheather Jrasiye na rekodi ya kupigwa hata pambano moja Jumapili iliyopita jijini Las Vegas nchini Marekani wakati wa Memorial Day Weekend.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo kwenye mgahawa wa FatBurger sehemu ulipotokea ugomvi, walidai kuwa chanzo ni mke wa T.I anayeitwa Tiny kuonekana   akiwa bege kwa bega  na Maywheather  kitendo kilichoonekana kumkera T.I na kuamua kumfuata bondia huyo sehemu aliyokuwa amekaa na kumuanzisha timbwili hali iliyopelekea mabaunsa kuingilia kati na kufanikiwa kuwatenganisha mastaa hao na kila mmoja kuchukua njia yake.

Tiny na Floyd Maywheather mke wa T.I mwanamama  ‘Tiny’ akimsikiliza kwa makini bondia Floyd Maywheather muda mfupi kabla ya tukio la ugomvi kutokea.

Baadhi ya vyanzo vimedai kuwa T.I amekuwa akitilia shaka ukaribu wa mkewe na Maywheather huku ikitajwa kuwa sio mara ya kwanza kwa Rapa huyo kumlalamikia Maywheather kutembea na mama watoto wake licha ya bondia huyo kukanusha mara zote na kudai kuwa  amekuwa akifahamiana  na Tiny kwa kitambo kirefu.

”I’m not sleeping with that girl [Tiny] and I told that man before. But if I was, talk to her about that, don’t talk to me about that. But I’m not going to be disrespectful because I’m not going to sleep with a married woman. Now if she was divorced”…alisema Maywheather

Tiny Fucking PostPichani ni Ujumbe na Picha aliopost mke wa T.I akifungukua kuwa yeye ni shabika mkubwa wa Maywheather na timu yake ya The Money Team(TMT)

Hata Hivyo imefahamika kuwa Tiny alikwenda mjini Vegas mwenyewe baada ya kupewa shavu la kusimamia mipango ya shereehe ya siku ya kuzaliwa ya binti wa bondia huyo  aliyepiga nae picha muda mfupi kabla ya ugomvi na kisha kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika ”My New Boo” kitendo kilichozidi kumtia hasira   mumewe.

Tazama Video hapo chini uone jinsi ugomvi ulivyokuwa

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s