REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA ULAYA, YAITANDIKA BAO 4 -1 ATLETICO

Diego Godin

Mchezaji wa Atletico Madrid, Diego Godin akishangilia baada ya kupachika goli la kwanza

Kikosi cha Real Madrid kinachonolewa na Kocha Carlo Anceloti hatimaye kimeweza kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kumi baada ya kuipa kipigo cha jumla ya  bao 4 – 1 timu ya Atletico Madrid katika mtanage uliochezwa katika  dimba la Estádio do Sport Lisboa nchini Ureno.

Atletico ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Madrid kupitia mchezaji wake ‘Diego Godin’ mnamo dakika ya 36′ kabla ya kusawazishwa na Sergio Ramos dakika za nyongeza kipindi cha pili cha mchezo na kufanya matokeo kuwa suluhu ya moja moja.

Hata hivyo kibao kiliwageukia mabingwa hao wa Hispania katika kipindi cha dakika 30′ za nyongeza,  baada kuruhusu  magoli matatu yaliyoipa tiketi ya ushindi Madrid huku yakifungwa na Gareth Bale DK ya 110′, Marcelo DK ya 118′ pamoja na mkwaju wa penalti uliopigwa na Straika Mreno ‘Cristiano Ronaldo’ baada ya kuangushwa.

Mashabiki wa Ral MadridMashabiki wa klabu ya Real Madrid wakiwa kwenye majonzi kabla ya timu yao kusawazisha.

Sergio Ramos

BEKI tegemezi wa Real Madrid, Sergio Ramos akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kusawazisha bao dakika za majeruhi za kipindi cha pili cha mchezo

 

Gareth Bale

STRAIKA wa Real, Gareth Bale akishangilia baada ya kupachika bao la Tatu

Cristiano RonaldoCristiano Ronaldo akifanya yake

Zidane na Carlo Anceloti

Madrid Mabingwa wa UEFA Iker Casillas

Wachezaji wa madrid wakiongozwa na kipa wa timu hiyo Iker Casillas aliyeshika kombe wakishangilia kunyakua ubingwa wa UEFA

Tazama Video za Magoli hapo chini…

                                

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s