50 CENT AKACHA MAHAFALI YA MWANAE, DOGO AMTOLEA UVIVU

'Marquise Jackson' & his Mother

Mtoto wa 50 Cent ‘Marquise Jackson’ akiwa na mama na dada yake kwenye mahafali.

Uchungu wa mwana aujuae mzazi lakini kwa Rapa 50 Cent  ameonekana kuupuzia msemo huo baada ya kukacha kuhudhuria mahafali ya mtoto wake wa kwanza wa kiume ‘Marquise Jackson’  aliyekuwa akihitimu masomo yake ya sekondari.

Akionekana kusikitishwa na kitendo alichofanya baba yake, Marquise alitupia picha akiwa amekumbatiana na dada yake na kisha kuandika ujumbe mzito uliosomeka

”Nilikuwa nahamu  kubwa ya kumuona baba yangu katika mahafali yangu lakini yeye hajaonyesha upendo. Dada yangu na mama daima wapo kwa ajili yangu jua wazi kwamba wewe haupo. Nimeifanya bila wewe.

Licha ya Hitmaker  wa 21Questions kutokutokea, Kijana wake aliweza kupata kampani kutoka kwa mama yake ‘Shaniqua’, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na anko wake Jim Jones.

Hata hivyo 50 amekuwa akiripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na mzazi mwenzake ikiwemo na kuripotiwa kumtumia mwanae ujumbe wa vitisho ingawa baadae alikanusha vikali habari hizo na kudai kuwa aliyekuwa akifanya hivyo ni mama wa mtoto huyo.

 

'Marquise Jackson''Marquise Jackson'1Hii ni moja ya picha aliyoposti Mtoto wa 50 Cent akiwa amekumbatia Dada yake iliyoambatanana ujumbe mzito.

Advertisements

One thought on “50 CENT AKACHA MAHAFALI YA MWANAE, DOGO AMTOLEA UVIVU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s