PIGO : MWIMBAJI NYOTA AMINA NGALUMA AFARIKI DUNIA

Amina Ngaluma

Amina Ngaluma enzi za uhai wake

Aliyewahi kuwa mwanamuziki wa dansi wa bendi za African Revolution ‘Wana tam tam’ na Double M, enzi hizo chini ya uongozi wa Muumin Mwinjuma, Amina Ngalum A.K.A Japanese amefariki dunia nchini Thailand, ambako alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki.

Mkurugenzi  wake wa zamani katika bendi ya Tam Tam, Asha Baraka, amesema kuwa Amina amefariki dunia wakati akifanyiwa upasuaji.

”Imeelezwa kuwa Amina alianza kuugua ghafla, huku akilalamika kuwa kichwa kinamuuna na tumbo, na ndipo alipokwenda hospitali kwa ajili ya kupima na kuambiwa kua alikuwa na uvimbe kichwani na hivyo kutakiwa kufanyiwa upasuaji,

Aidha ilielezwa kuwa uvimbe huo ulikuwa ukitoa damu na baada ya kuanza kufanyiwa upasuaji hakuweza kuamka tena na ndipo umauti ulipomfika”. alisema Asha Baraka.

Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors. Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam.

Habari na sufiani mafoto

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s