DIAMOND AZIDI KUNG’ARA, ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET AWARDS 2014

Diamond BET Awards 2014Tangu aweke rekodi ya kuzoa tuzo 7 za KTMA pamoja na kuchaguliwa kuwania Tuzo za KORA na zile za  MTV MAMA, mshika kipaza wa Tanzania  ‘Diamond Platnumz’ ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kuchaguliwa kwa  mara ya kwanza kuwania Tuzo kubwa kabisa za watu weusi zinazofahmika kama BLack Entertainment  Awards maarufu kama BET  huku akiwa msanii pekee anayetokea Afrika Mashariki.

Katika Tuzo hizo,  Diamond  anawania  kipengele cha ‘Best International Act’  akichuana vikali na wakali kama vile  ‘Davido’ kutoka Nigeria, kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage kutoka Nigeria pamoja na Toofan wa Togo.

KWA SASA SINA MENGI YA KUSEMA,ILA NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA HATUA HII,NA SIWEZI SAHAU KUWASHUKURU MASHABIKI WANGU KWA SUPPORT MNAYONIPA NA KUNI MOTIVATE NIZIDI KUFANYA VIZURI KILA SIKU,NINA IMANI MDA SIYO MLEFU MZIKI WETU UTASOMEKA KWENYE RAMANI TUNAYOITAKA,NIWAKUMBUSHE TU,HIZI NI NOMINEES HATUA ZA UPIGAJI KURA ZIKIANZA NITAWAJULISHA.USISAHAU TU KUENDELEA KUNIPIGIA KURA TUZO ZA MTV MAMA,PIA KORA KWA KULIKE PAGE YAO NA KU COMENT JINA LANGU.AHSANTENI.aliandika Diamond kwenye ukurasa wake wa Facebook wenye wafuasi zaidi ya Laki na nusu . 

Kilele cha Tuzo za BET  ni  Jumapili ya June 29 mwaka huu mjini Los Angels Marekani . KWa pamoja Watanzania tunaweza kumpigia kura kwa wingi Diamond ili kumuwezesha kunyakua Tuzo hizo zote kubwa anazowania kwa hivi sasa…

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s