MASHABIKI 15 WAFARIKI DUNIA KWENYE MECHI YA TP MAZEMBE NA AS VITA NCHINI CONGO

TP Mazembe

Polisi wakiwarushia mabomu ya machozi mashabiki

Mashabiki 15 wa soka wamekufa kwa kukanyagana baada ya polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi kwenye kundi la watu kwenye uwanja wa soka  wa  Stempede uliopo katika jiji la Kinshasa, jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa jeshi la  polisi nchini humo wamesema  mashabiki walipatwa na hasira jana jioni baada ya timu yao ya AS Vita Club kuchapwa kwa bao moja kwa sifuri na klabu ya Tp Mazembe toka mji wa Lubumbashi .

Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza na kikosi cha msalaba mwekundu

Kiongozi mmoja wa mjini huko ‘Emmanuel Akweti’ amesema askari polisi wanne walibughudhiwa na mashabiki na walipofyatua mabomu ya machozi ndipo mashabiki hao wakaanza kukimbia na kukanyagana hali iliyopelekea kusababisha vifo.

Aliongezea kwa kusema kuwa watu hao 15 wamekufa kwa kukosa hewa na wengine zaidi ya 24 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s