KUNDI LA BOKO HARAM WAONYESHA WASICHANA WALIOWATEKA

Boko HaramKiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.

Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.

Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake mia moja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Wakati huohuo Waziri wa mambo ya ndani nchini Nigeria amesema serikali haitakubali masharti ya kundi la Boko Haram kwamba kwanza liwaachilie wapiganaji wake kabla ya wasichana zaidi ya miambili waliotekwa nyara waachiliwe.

Waziri Abba Moro amsema ni jambo la kipuuzi sana kwa kundi la kigaidi kujaribu kuweka masharti kama hayo.

Wasichana watatu kati ya waliooyeshwa na kuongea katika kanda hiyo walikuwa wanavalia hijabu. Mmoja alisema kuwa amesilimu wakati mwingine akisema yeye tayari ni Muisilamu.

CREDITS : BBC SWAHILI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s