WAMBURA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KITI CHA URAIS SIMBA SC

Michael WamburaWanachama wa klabu ya wekundi wa msimbazi Simba wameendelea kumiminika kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kupitia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.

Huku aliyewahi kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo na shirikisho la soka Tanzania  ‘Michael Richard Wambura’ kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ambayo pia inawaniwa na Evans Kaveva na Andrew Tupa baada ya kukamilisha zoezi hilo wanachama wanaomuunga mkono Wambura waliweza kumuombea dua mgombea wao.

‘’Kuchukua kwangu fomu leo ni katika harakati za kuhitimisha miaka 78 ya Simba kuendelea kutegemea watu fedha za mfukoni, tunahitimisha mfumo ambao hauupeleki klabu ya Simba kujitawala kwa misingi ya kiuchumi, kwa misingi ya kimashindano, wote tunaona na wote tumeona kwa kipindi kirefu jinsi klabu yetu ilivyo’’ alisema Wambura.

Baada ya Wambura, ulifuata msafara wa Evans Aveva ambaye amerudisha fomu aliyochukua jana ya kuwania urais ambapo msafara wake umeongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali ulioanzia mtaa wa Lumumba na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wamefurika nje ya jengo makao makuu ya klabu hiyo na kisha alifuata mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais Bwana Swedi Mkwabi.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s