MMILIKI WA LOS ANGELS CLIPPERS ‘DONALD STERLING AWAOMBA RADHI MASHABIKI

Donald Sterling

Donald Sterling

Mmiliki wa klabu ya mpira wa kikapu ya Los Angels Clippers ‘Donald Sterling’ ameomba radhi mashabiki kwa matamshi yake ya kibaguzi aliyomtolea mpenzi wake.

Shirikisho la mchezo huo nchini Marekani lilimpiga marufuku mmiliki huyo ya kutohudhuria mazoezi ya Clippers pamoja na mechi zake sambamba na kutohusika katika maamuzi yoyote ya ndani ya timu hiyo ikiwa na kulimwa  faini ya dola za kimarekani milioni 2.8.

Hata hivyo Sterling alikiambia kituo cha televisheni cha America Tv ya kwamba alifanya kosa kubwa sana ambalo hata hajui anavyoweza kulirekebisha .

Kauli hiyo inakuwa ni ya kwanza kutolewa na Sterling tangu kutokea kwa sakata hilo ambapo alikuwa akimkaripia mpenzi wake kwa kumtaka kutojihusisha na watu weusi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s