THAILAND YAMSHITAKI RASMI WAZIRI MKUU WAKE ‘YINGLUCK SHINAWATRA’ KWA TUHUMA ZA UFISADI

Yingluck Shinawatra

Yingluck Shinawatra

Tume ya kupambana na ufisadi nchini Thailand imemshitaki rasmi waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Yingluck Shinawatra kwa madai ya kupuuza jukumu lake katika usimamizi wa mpango uliokosolewa vikali wa kutoa ruzuku ya mchele.

Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama ya katiba kumuondoa madarakani waziri mkuu huyo ambaye anatuhumiwa kwa kuruhusu mpango huo wa mchele uliokuwa sera muhimu katika utawala wake kuendelea licha ya kushauriwa kwamba ulikuwa ukitumiwa vibaya na kuzongwa na ufisadi.

Uamuzi huo unamaana kuwa mwanamama YingLuck atakabiliwa na kura ya kumng’oa madarakani katika baraza la seneti ikiwa theluthi tano ya kura zitaunga mkono uamuzi wa kumtia hatiani na anaweza kuzuiwa kushiriki katika masuala ya  siasa kwa miaka mitano.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s