CHAMA CHA ANC CHASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MKUU WA URAIS NCHINI AFRIKA KUSINI KWA ASILIMIA 63

Chama cha ANC chashinda
Wakuu wa tume ya uchaguzi nchini Afrika-Kusini wametangaza kuwa shughuli ya kuhesabu kura inaenelekea kukamilika baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi kwa mara ya tano tangu utawala wa mwafrika mzungu.

Chama tawala cha ANC kinaongoza kwa zaidi ya asilimia 63, huku kile cha Democratic Alliance kikiwa na asilimia 23.
Chama kipya cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kikiwa katika nafasi ya tatu.
Jumla ya asilimia 96 ya kura zilizopigwa zimehesabiwa.
 
Mwandishi wa BBC Andrew Harding anasema kuwa ukosefu wa ajira,ufisadi na ukosefu wa usawa katika jamii ni changamoto kubwa lakini wapiga kura bado wana imani na chama cha African National Congress ANC.
 
Tume ya uchaguzi imesema kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani katika maeneo mengi ya nchi huku asilimia 73 ya wapiga kura wakijitokeza kupiga kura.
 
Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu nchi hiyo kuondokewa na rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo hayati Nelson Mandela. Afrika Kusini imetimiza miaka 20 tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu.
 
Idadi kubwa ya wananchi imekuwa ikilalamikia utenda kazi wa serikali hasa kwa kuwa kuna kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.
 
Wadadisi wanasema kuwa chama cha ANC huenda kikatumia fursa hii kuimarisha uchumi wa nchi hasa baada ya miaka mitano ya kile kinachosemekana kuwa utawala mbovu wa Rais Jacob Zuma.

-BBC

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s