MARTIN KADINDA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BIFU LA WEMA NA KAJALA

Wema na KajalaMbunifu wa mavazi Tanzania ‘Martin kadinda’ AKA Mzee wa kwachukwachu au ‘The Buttonist’ amefunguka kwa mara ya kwanza laivu pasi na kupepesa, kuhusiana na vuguvugu la kutokuwa na maelewano mazuri baina ya Waigizaji wa filamu Wema Sepetu na Kajala wanaodaiwa kutopikia chungu kimoja hivi sasa.

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya Endless Fame, mbunifu huyo  ambaye pia ni meneja wa Wema Sepetu ‘Madam’,  alisema kwamba mitandao ya kijamii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa tofauti baina ya mastaa hao wawili.

Aliongezea kuwa hata wale  wanaojiita Team Wema  waliopo kwenye mtandao wa Instagram hawana mawasiliano nao  na isitoshe  hakuna mtu anayewatuma au kuwashinikiza, bali hufanya vile kwa matakwa yao na wao kama Endless hawawezi kuingilia uhuru wa mtu binafsi. Unaweza ukasoma hapo chini alichoandika kaka meneja huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram…

”Good morning all of You…. I just woke up Like “Hasiraless” kwakuwa hili vugu vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu endless fame….

katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili… lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza….

yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu.. kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi… ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space…… tukawa tumefunga mjadala huo……

endless fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala na mtu yoyote…. endless fame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki…

hapana hapana… Hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona. Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema.

Team wema wote waliopo insta sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati Kwa wema… Poleni Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi.Tusiishi fake life in instagram while in really hatuna hata hela ya chumvi

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s