KIMENUKA MBAYA , POLISI NCHINI BRAZIL WAGOMA WAKIDAI NYONGEZA YA MSHAHARA

Polisi wagoma BrazilZikiwa zimesalia takribani siku 34 kuweza kuanza rasmi kwa michuano ya kombe la Dunia,  polisi nchini Brazil wamefanya mgomo wa saa 24 Jumatano iliyopita katika miji kadhaa nchini humo ukiwemo mji mkuu wa ‘Rio De Janeiro’ ambao utaandaa mechi saba ikiwemo  fainali ya kombe  hilo itakayochezwa Julai 13 wakidai  mazingira bora ya utendaji kazi. 

Shirikisho hilo la polisi limefanya maandamano ya amani huku msemaji wa jeshi hilo Renato Deslandes akinukuliwa na BBC akisema kwamba Polisi wataendelea na mgomo katika kipindi cha wiki za mbeleni ambapo michuano hiyo itakuwa tayari imeshaanza kutimua vumbi endapo kama serikali haitaongeza kuwalipa kulingana na mfumo wa bei ulivyo kwa hivi sasa.

Aliendelea kusema kuwa mishahara  wanayolipwa hivi sasa inacheza kati ya dola za kimarekani 3,200 mpaka 5800 kabla ya kukatwa kwa kodi na ulinzi jamii na kuongezea kwamba tangu kutokea kwa mfumo wa bei   mishahara yao haikuweza kupandishwa.

Wakati hayo yakiendelea, kocha mkuu wa Brazil ambao ni wenyeji wa michuano hiyo ‘Luiz Filipe Scolari’ amekizindua kikosi chake kitakachoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho huku akiweka wazi majina ya wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi hiyo katika fainali za Dunia mwaka huu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s