DR. DRE : MIMI NI BILIONEA WA KWANZA KATIKA HIP HOP, BAADA YA APPLE KUPANGA KUINUNUA KAMPUNI YAKE YA BEATS ELECTRONICS

DreRapa na Mtayarishaji wa muziki  Andre Romelle Young’   maarufu kwa jina la steji Dr.Dre amesema kuwa  yeye ni bilionea wa kwanza katika Hip Hop kufuatia  kampuni ya Apple kutangaza kuinunua kampuni yake ya Beats Electronics inayotengeneza Headphones za Beats by Dre.

”Bilionea wa kwanza katika Hip Hop kutoka West Coast (alafu akatia na kionjo cha tusi)” alisema Dre katika video fupi aliyochukulia na staa wa  filamu za fast & Furious muigizaji Tyrese Gibson.

Katika Video hiyo Tyrese alikuwa akijadili kuhusiana na orodha iliyotolewa na jarida la Forbes ya wasanii wa Hip hop wanaoongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu.

”Haiwezekani” Tyrese anasema orodha ya Forbes imebadilika ghafla” ”kwa hatua kubwa” aliongezea Dre.

Kama ilivyoripotiwa hapo jana(May08) na mtandao wa gizmodo uliosema kwamba Apple imepanga kuinunua Beats Electronics inayomilikiwa na Dre pamoja na Jimmy Iovine kwa gharama ya dola za kimarekani Bilioni 3.2 huku dola bilioni 1 zikitajwa  kuingia  mfukoni mwa mtayarishaji huyo..

Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha  CNBC walisema  kwamba ununuzi huo unakwenda kinyume na sera za muanzilishi wa kapuni hiyo Steven Jobs aliyefariki Dunia mwaka 2011,  zilizokuwa zikipinga  ununuzi wa vitu vyenye gharama kubwa.

Dre anayeshikilia nafasi ya pili hivi sasa kwa wasanii wa Hip Hop wenye hela ndefu huku utajiri wake ukitajwa kufikia dola milioni 550 akiwa amemzidi Jay Z kwa tofauti ya dola milioni 30. Hiyo ni kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Forbes…

“I don’t really care about any of that,” “Jay Z is my guy, man. I love him to death.”  alisema Dr.Dre baada ya kupigwa swali na muandishi kuhusiana na anavyojisikia kuwa juu ya Jay Z

Tazama Video fupi hapo chini umsikilize alichosema Dre baada ya kupata shavu hilo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s