RAY C HOI HOSPITALI AKISUMBULIWA NA UGONJWA WA DENGUE

Ray C Dengue

Mwanamuziki Ray C akiwa Kitandani baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa Dengue

Msanii nguli wa muziki Tanzania, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C au kiuno bila mfupa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa Dengue  ambao umepata umaarufu wa ghafla na kuwa ndio habari ya mjini kwa hivi sasa hasa kutokana na kuambukiza idadi kubwa ya wakazi waishio jijini Dar es salaam   huku dalili zake zikitajwa kufanana na zile za Malaria.

“Tumemfanyia vipimo, ana homa kali sana lakini hana malaria. Baada ya kuchunguza dalili, tumechukua vipimo na kubaini kwamba amepata maambukizi ya dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu kwa sasa,” alisema  daktari mmoja aliyekuwa zamu ambaye hakupenda kutaja jina lake, wakati akimweleza mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanaspoti kuhusiana na hali ya mwanamuziki huyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na madaktari mbalimbali, wanaielezea Dengue kama ugonjwa unaosambazwa na mbu  mweusi aina ya  Aedes Egypitia ambaye  hueneza virusi vya ugonjwa huo hasa majira ya asubuhi na jioni.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s