#BRINGBACKOURGIRLS : MASTAA WA NIGERIA WAUNGANA NA WAANDAMANAJI KUISHINIKIZA SERIKALI KUWAREJESHA WANAFUNZI WA KIKE 234 WALIOTEKWA NA BOKO HARAM

Banky W Vilio vya wazazi bado vinaendelea nchini Nigeria kufuatia tukio la mabinti  wapatao 200 waliokuwa wakisoma katika shule moja ya bweni iliyoko katika mji mkuu  wa Abuja,  eneo la Chibok katika kitongoji cha Borno kutekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram.

Masupastaa wengi nchini humo tayari wameshajiunga kwenye kampeni iliyopewa jina la #BringBackOurGirls inayohamasisha kikundi hicho kuwaachia huru wasichana hao waliowashikilia wanaokadiriwa kufikia 234 wakiwa salama,  kwani kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu

Mastaa kama vile Banky W, Waje, Yemi Alade, Lami Phillips na msanii wa  filamu kutoka Nollywood Omoni Oboli mnamo may 05 waliungana pamoja na wakazi wengine katika eneo la Allen Avenue na kutengeneza kundi la  wakazi waishio mjini Lagos ambao wote kwa pamoja waliweza kuandamana mpaka  ikulu ya Lagos iliyopo katika eneo la Alausa huku wakiimba nyimbo na kuishinikiza mamlaka husika ichukue hatua za haraka ili kuweza kutatua kilio hicho kinachoongelewa na vyombo mbalimbali vya habari Duniani huku kukiwepo na taarifa kuwa hata wiki iliyopita mastaa wengine akiwemo Waje na Seun Kuti nao pia  waliandamana

PhillipsLami Phillips

Bring Back Our GirlsBanky W, Yemi Alade, Waje pamoja na waandamanaji wengine wakielekea eneo ilipo ikulu ya Lagos

In Nigeria Bring Back Our DaughtersWanaharakati na mabango yao yakiwa yamebeba ujumbe tofauti tofauti

Lagos HouseWaandamanaji baada ya kuwasili katika viunga vya ikulu

 Drake

 

Rapa wa marekani ‘Drake’ nae ni miongoni mwa mastaa wakubwa Duniani wanaoiunga mkono    kampeni hiyo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s