MAN UNITED YAIPA KIPIGO CHA BAO 3 – 1 HULL CITY.

James WilsonIkiwa ni mchezo wake wa  tatu  tangu kukaimu kiti cha  David Moyes,  kocha wa muda wa Manchester United ‘Ryan Giggs’  amefanikiwa kuipa kipigo cha mabao 3 – 1 klabu ya Hull City katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Old Trafford mapema  hapo jana.

Kinda mdoog kabisa wa United aitwae ‘James Wilson’ ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Hull City baada ya kupachika mabao mawili peke yake  kabla ya mshambuliaji hatari wa mashetani hao ‘Robin Van Persie’ kufunga bao la Tatu  mnamo dakika ya themanini na saba huku bao  pekee la Hull City likifungwa na Matt Fryatt na kufanya matokea kuwa Tatu kwa moja.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Manchester kuendelea kubaki katika nafasi yake ya saba iliyokuwepo hapo awali ikiwa na pointi 63 huku ikiwa imebakiza   mchezo mmoja tuu mkononi  kuweza kumalizika kwa ligi kuu hiyo ya England maarufu kama EPL..

James Wilson Manchester UnitedJames Wilson akitupia wavuni shuti kali kwa mlinda mlango wa Hull City

JWilson na RVPWilson na Van Persie wakipongezana

Frayatt wa Hull CityMatt Fryatt wa Hull City akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kupachika bao pekee dhidi ya United.Tazama video ya magoli hapo chini

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s