VIDEO : KANYE WEST AMPA SHAVU LA KUMSIKILIZA SHABIKI ALIYEDAI ANAUWEZO WA KUCHANA ZAIDI YAKE

 KanyeKanye akimsikiliza shabiki aliyekuwa akiimba mbele yake.

Rapa na Mmiliki wa lebo ya GOOD Music ‘Kanye West’  mwishoni mwa wiki aliamua kumpatia nafasi ya kumsikiliza shabiki  mmoja aliyeonekana kuwa msanii asiye na jina wa miondoko ya kufokofoka, wakati  alipokuwa akirudi kwenye makazi yake aliyokuwa amepanga ya Soho eneo la west Hoolwood, mjini Los Angels, Marekani,

Akiwa ameongozana sambamba na mpenzi wake Kim Kardashian, kijana mmoja aliwafuata kwa nyuma na kudai kuwa yeye ni mkali na angependa adhihirishe uwezo aliokuwa nao mbele ya rapa huyo na baada ya kupewa nafasi, msanii huyo aliweza kuimba kwa mtindo wa freestyle hali iliyomvutia  kanye na kumfanya  asimame pembezoni mwa nyumba yake huku akimsikiliza na baada ya jamaa huyo kumaliza, Kanye alimwambia amefanya vizuri lakini kwa wakati huo anahitaji kwenda kupumzika.

Mpaka hivi sasa bado haijaweza kufahamika hatma ya shabiki huyo kama ataweza kulamba shavu la kusainiwa kwenye lebo ya rapa huyo  licha ya uwezo wa hali ya juu aliounyesha pasipo kujali uwepo wa  kamera nyingi zilizokuwa zikimmulika kipindi anachana mbele ya hitmaker huyo wa Bounce.

 Unaweza ukatazama hapo chini Tukio zima lilivyokuwa, sio mchezo kumfata mtu kama Kanye West ambaye ni miongoni mwa marapa wa kubwa na wenye mkwanja mrefu, lakini huyu jamaa aliweza ingawa hii sio mara ya kwanza kwani hata mwanamuziki Big sean aliweza kupata shavu la kujiunga na Good Music kwa staili inayofana na hii

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s