LIVERPOOL YASHIKWA SHATI NA PALACE, YALAZIMISHWA SARE YA BAO 3 – 3

  Luis Suarez akishangilia bao lake Mshambuliaji wa Liverpool ‘Luis Suarez’ akishangilia bao lake dhidi ya Crystal Palace.

Mcheza kwao  hutunzwa, Klabu ya Crystal Palace iliyowakaribisha kwenye uwanja wao wa nyumbani majogoo wa jiji la London, Timu ya Liverpool na kufanikiwa  kuwatoa kijasho chembamba  katika mtanange uliokuwa wa vuta nikuvute uliopelekea  kuzififisha ndoto za kuchukua ubingwa wa ligi kuu kwa miamba hiyo ya soka barani Ulaya.

Liverpool  ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Palace kupitia wachezaji wake Joe Allen aliyefunga goli la kwanza, akifuatiwa na  Daniel Sturridge pamoja na Luis Suarez.

Gayle vs LiverpoolDwight Gayle wa Palace akishangilia kwa furaha goli la tatu alilowachapa Liverpool

lakini hali ya mchezo ilibadilika ghafla baada ya magoli ya mfululizo yaliyofungwa dakika za lala salama na  Damien Delaney mnamo dakika ya 79′, Dwight Gayle 81′ na 88′  wa Crystal Palace yaliweza kabisa  kugeuza matokeo na kuwa suluhu ya goli 3 – 3.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool iwe na Pointi 81 tofauti ya pointi 1 na Man City, huku ikiwa imebakiza mchezo mmoja mkononi dhidi ya NewCastle United utakaochezwa  jumapili ya May 11 wakati mpinzani anayemfuatia timu ya manchester City ikiwa na pointi 80 huku ikiwa  imebakiza michezo miwili kuweza kufungwa kwa pazia la ligi kuu ya England EPL.

Kwa maana hiyo endapo manchester City ikafanikiwa kushinda michezo yake yote  miwili iliyosalia, ukiwemo  dhidi yake na  Aston Villa utakaochezwa  Ijumaa ya May 7 pamoja na ule wa West Ham utakaochezwa Jumapili ya may 11 bila shaka atakuwa amezima ndoto za vijana wa Anfield za kuweza kunyakua ubingwa huo.

Palace

Liverpool PlayersWachezaji wa Liverpool wakiwa hawaamini kilichowatokea baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya goli 3 – 3.

Tazama Video za magoli hapo chini…

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s