HIVI NDIVYO DIAMOND ALIVYOWASHUKURU MASHABIKI WALIOMUWEZESHA KUNYAKUA TUZO 7 ZA KTMA 2014

Diamond Platnumz

Daima mtu anayepewa chakula na baada ya kushiba akasema asante huyo anachukuliwa kuwa ni muungwana, hivyo ndivyo alivyofanya Rais wa serikali ya watu wasafi Tanzania, Diamond Platnumz aliyeweka Rekodi ya kuwa msanii pekee wa kwanza Tanzania kuweza kunyakua Tuzo nyingi za  Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 tangu kuanzishwa kwake yapata miaka  14 iliyopita.

Ushindi huo wa kishindo umemfanya Diamond avunje rekodi zilizowahi kuwekwa na kaka zake akiwemo mwanamuziki 20 Percent na  bendi ya mashujaa waliopata Tuzo tano tano kila mmoja mnamo mwaka 2012 .

Akionyesha kuwa mwenye wimngi wa furaha, Diamond aliandika kupitia ukurusa wake wa Facebook aliweza kuwashukuru mashabiki wake walioweza kumpiga kura na kuibuka kidedea katika Tuzo hizo.

”Hakika ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini kwa uwezo wa mwenyez mungu ametufanyia wepesi na hatimaye kufanikisha… Nawashkuru sanasana Mashabiki zangu wote kwakuwa nyie ndio mlionipa tuzo hizi kupitia kura zenu… Family, uongozi wangu.. bila kuvisahau vyombo vyote vya habari vilivyo fanya kazi zangu zisikike kila kona”. aliandika Diamond..

Aliongezea ”Niwashkuru pia wasanii wenzangu, kwakuwa naamini wote walifanya kazi nzuri na ndiomaana wote tukawa pale ila kwakuwa mshindi ni mmoja, ikatokea kuwa bahati yangu…Ahsanteni sana, cha mwisho nnachoweza kusema tu ni kwamba (Tika! Tika!) yaani (Saba saba) Nomination 7 Tunzo 7…! tuhamieni MTV Awards tuilete Heshima nyumbani sasa”.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s