PICHA : MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AONGOZA MAELFU YA WAISLAMU KATIKA MAZISHI YA SHEIKH ILUNGA JIJINI DAR LEO

Lipumba na Maalim Seif

Pichani ni makamu wa Rais wa kwanza wa   Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba katika mazishi ya Sheikh Ilunga kwenye makaburi ya Mwinyimkuu.

Sheikh Ilunga alifariki usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari kwa muda mrefu.

Maandalizi ya maziko yake yalifanyika katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam.

Katika dua hiyo iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na Shuura ya Maimamu,ilihudhuriwa na Waislamu wengi waliofurika msikitini huku wengine wakikosa nafasi ndani na kulazimika kuswali nje.

Viongozi mbalimbali wa Kiislamu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara  na visiwani Zanzibar walishiriki.

Makamu wa wa kwanza wa Rais wa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa ni kiongozi pekee wa Serikali aliyeshiriki maziko hayo kuanzia hatua ya mwanzo hadi mwisho.

Maziko yake Sheikh ilunga yaligusa hisia za wengi kiasi cha watu wengine kushindwa kujizuwia na kutokwa machozi.

Akiwahutubia maelfu ya Waislamu walioshiriki maziko hayo makaburini,Sheikh Ally Bassaleh aliwataka Waislamu kuiga ujasiri wa Sheikh Ilunga huku akisema kwamba wingi wa watu walioshiriki msiba huo ni ishara ya wazi kwamba Sheikh ilunga alikuwa anafanya kile ambacho waislamu wanakitaka.

Sheikh Ilunga enzi za uhai wake aliwahi kutafutwa na Serikali ya Tanzania  kwa madai ya kufanya uchochezi. Aidha mwaka jana serikali kupitia Jeshi la Polisi lilitangaza kwamba atakaye kutwa na kanda,cd na dvd za Sheikh Ilunga atakamatwa.
Sheikh IlungaMaalim Seif Sharif Hamad akiongea na waumini wa dini ya kiislamu  waliohudhuria mazishi ya sheikh Ilunga katika  msikiti wa Kichangani Magomeni jijini Dar es salaam.

Mazishi ya Sheikh IllungaMaelfu ya Waumini wakielekea makaburini

Mazishi ya Sheikh Illunga Dar

 

Waumini wakiwa nje ya msikiti wa Kichangani magomeni baada ya kukosa siti ndani.

Kaburi la Sheikh IlungaKaburi alilozikwa Sheikh Ilunga.

Safari ya mwisho ya sheikh IllungaWaumini wakiuweka vizuri mwili wa Sheikh Ilunga kaburini kwake.

Maalim Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh wa Ilunga Shekh.Hassan Kapungu yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam. akijumuika na Wanancjiji Dar-es-Salaam.

 

Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.

Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam. (Picha na Salmin Said OMKR)

Unaweza pia ukatazama dawa alizokuwa akitoa Sheikh Ilunga enzi za uhai wake hapo chini

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji’un

Chanzo  :  muniramadrasa.blogspot.com

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s