FLOYD MAYWHEATHER AMCHAPA MAIDANA KWA MBINDE

Maywheather Vs Maidana

Bondia Tajiri, sugu na asiyekuwa na rekodi ya kupigwa hata pambano moja tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa, Floyd Money Maywheather(37) alifajiri ya jana aliweza kumpiga kwa mbinde  bondia muagentina Marcos Maidan katika mpambano uliofanyika  kwenye ukumbi wa MGM-Grand Arena mjini Las Vegas, Marekani katika pambano la raundi 12.

Katika pambano hilo lililokuwa la uzito wa ‘Welterweight, Maywheather ni bingwa anayeshikilia mikanda mikubwa ya WBC na WBA alijikuta akipewa wakati mgumu dhidi ya mpinzani wake  Maidana aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kufanikiwa kumpitishia makonde mazito yaliyoweza kumuingia vizuri maeneo ya kichwa kati ya raundi ya kwanza mpaka ya nne hali iliyompa upinzani mkali bondia huyo wa Marekani.

Floyd Maywheathe Vs MaidanaMaywheather akimrushia konde mpinzani wake Maidana

Hata hivyo hali ya mchezo ilibadilika mnamo raundi ya sita baada ya Maywheather kubadilika na kuanza kuonyesha makali yake yaliyompelekea aibuke mbabe wa pambano hilo kwa jumla ya ponti 117 kwa 113 alizopewa Maidana,huku  jaji wa kwanza akitoa pointi 114 – 114, wa pili akitoa pointi 117 kwa 113 na wa tatu 116 – 112 na kupelekea ushindi kwenda kwa mmarekani huyo kwa tofauti ya pointi kiduchu mno.

Maywheather alisema kwake lilikuwa ni pambano zito na kuahidi kurudiana na muagentina huyo mwezi septemba. Kwa upande wa Maidana alijigamba kwa kusema kuwa alistahili kuwa mshindi kufuatia makonde yenye ujazo aliyoweza kumpenyezea na kudai kuwa yupo tayari kwa mchezo wa marudiano.

Maywheather kazini na MaidanaMaywheather Vs Maidana1jb & Maywheather

Mwanamuziki Justin Bieber akimpongeza mshikaji wake Maywheather baada ya kushinda mpambano huo

TMTMGM Maywheather Vs Maidan123Kushoto ni mabondia maywheather na Maidana wakionyesha mikono juu kuashiri kumalizika kwa pambano lao, kulia ni Maidana akiwa amebebwa na kocha wake

TMT

Tazama video ya pambano hilo lililovyokuwa hapo jana

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s