JUSTIN BIEBER KUMSINDIKIZA BONDIA FLOYD ‘MONEY’ MAYWHEATHER KATIKA PAMBANO LAKE LA LEO DHIDI YA MAIDANA

Floyd Maywheather & Justin BieberMwanamuziki Justin Bieber atamsindikiza kwa mara nyingine tena rafiki yake kipenzi  bondia ‘Floyd Money Maywheather’ katika mpambano wake wa leo usiku dhidi ya muagentina ‘Marcos maidana’ utakaochezwa katika  ukumbi wa MGM Grand garden Arena  mjini Las Vegas marekani.

Maywheather anatamba na rekodi ya kutowahi kupoteza pambano tangu aanze ngumi za kulipwa. Mashabiki wengi wa masumbwi Duniani wamekuwa wakijiuliza kama rekodi hiyo itavunjwa na Maidana hii leo.

Ukiachilia mbali na Justin Bieber, Kruu nzima ya Maywheather inayofahamika kwa jina la ‘The Money Team’ itakuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya kumpa kampani bondia huyo anayeshikilia mataji makubwa mbalimbali ya mchezo wa ngumi Duniani.

Taarifa zinasema kwamba mpambano huo utamfanya Maywheather aweke kibindoni kiasi cha dola za kimarekani milioni 32(Tsh Bilioni 51) wakati mpinzani wake akiondoka na kitita cha  dola milioni 1.5(Tsh bilioni3 ).

Hii sio mara ya kwanza kwa Justin Bieber  kumsindikiza bondia huyo, kwani imekuwa ni kama desturi kwa baadhi ya wasanii nyota kumsindikiza mkali wao huyo, miongoni wao ni pamoja na  Lil Wayne, 50 cent na familia ya YMCMB kwa ujumla.

Maidana Vs MaywheatherBondia Marcos maidana(Wa kwanza kulia) na Floyd Money maywheather (Wa kwanza Kushoto) wakipima uzito kwa ajili ya mpambano wa hii leo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s