VIDEO MPYA YA SAUTI SOL ‘NISHIKE’ YAFUNGIWA KUCHEZWA KWENYE VITUO VYA TV NCHINI KENYA

Sauti SolIkiwa ni siku mbili zimepita tangu Video mpya ya kundi la Sauti Sol inayoitwa ‘nishike’ kuachiwa ,mamlaka ya  Kenya imeifungia video hiyo kuonyeshwa kwenye vituo vya televisheni nchini humo kwa kile kilichodaiwa kuwa na picha nyingi zisizokuwa na maadili.

Akifafanua suala hilo hapo jana kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Mdundo,  kiongozi kinara wa kundi hilo aitwae ‘Bienaime’ alisema video yao  imefungiwa kutokana na  kuonyesha picha ambazo hazifai kutazamwa na watu walio na umri chini ya miaka 18.

Hata hivyo Bien aliwashukuru mashabiki kwa mchango wao mkubwa walioutoa wa kuitazama video hiyo kwenye akaunti yao ya Youtube iliyo na  jumla ya video 17 na kuifanya kuwa miongoni mwa video zilizotazamwa zaidi katika kipindi kifupi tangu iwekwe ikiwa tayari imeshatazamwa   na watu zaidi ya laki moja.

Wakili wa bendi ya Sauti Sol amepanga kufikisha mahakama malalamiko ya wateja wake ili kuweza kuachiwa huru kwa video hiyo sambamba na kuendelea kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni.

Hii sio mara ya kwanza kwa video za nchini Kenya kufungiwa, kwani hata kundi la P-Unit liliwahi kukumbana na adhabu hiyo kali kufuatia video ya wimbo wao wa ‘You Guy(Dat Dendai)kufungiwa licha ya kuchukua Tuzo ya Channel O kama  video bora ya Afrika Mashariki

Itazame hapo chini video ya Sauti Sol iliyopigwa Ban

 

  

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s