CHELSEA NJE UEFA CHAMPIONS, YALOWESHWA BAO 1 – 3 TOKA KWA ATLETICO MADRID

Wheeling way: Atletico's Turkish midfielder Turan celebrates his goal which books his side's final berth

Kiungo wa Atletico Madrid Turan akishangilia bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea

Chelsea imejikuta ikichezea kipigo cha mabao 1 – 3 kutoka kwa Atletico Madrid ya Hispania katika mtanange uliochezwa kwenye uwanja wa  Stamford Bridge usiku wa leo na kufuta  matumaini ya kucheza fainali ya michuano hiyo.

Licha ya kutangulia kuziona nyavu za wapinzani wao, haikuweza kuwa muarobaini kwa kwao kuzuia kipigo kilichoifanya Atletico ipige hatua moja mbele na kufuzu hatua ya fainali.

Argy bargy: John Terry squares up to some of the Atletico players as tempers fray ahead of the penalty

Mtu mzima John Terry akizozana na wachezaji wa Atletico

Bao la kwanza la Chelsea liliwekwa kimyani na Straika ‘Fernando Torres’ kabla ya Adrian wa Atletico kusawazisha dakika moja kabla ya kuelekea mapumziko

Hali ilizidi kuwa tete zaidi kwa vijana wa Mourinho,  baada ya kuruhusu magoli mengine kupenya kwenye ngome yao, yaliyopachikwa na Diego Costa kwa mkwaju wa penalti na lingine likifungwa na Arda Turan.

Goal-bound: Torres scores to give Chelsea the early 1-0 lead to the delight of the home fans

Straika wa Chelsea akipiga kwa ustadi kabisa mpira kwenye lango la Atletico lililoweza kuzaa goli.

Atletico itavaana na Real Madrid kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Jumamosi ya May 24 katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Estadio Do Sport Lisbon, Ureno.

Kama ulikosa kutazama mchezo huo, video za magoli ziko hapo chini. Poleni Mashabiki wa Chelsea..Asiyekubali kushindwa sio mshindani.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s