AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI MWINGINE TOKA YANGA, NI KIUNGO FRANK DOMAYO, ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI

FRANK DOMAYO

Frank Domayo akisaini mkataba na Azam Fc

Ikiwa yamepita takribani masaa 48 tangu mshambuliaji jembe na tegemezi wa Yanga ‘Didier Kavumbangu’ amwage wino wa kuichezea  Azam Fc kwa mkataba mmoja, mchezaji mwingine wa wana Jangwani anayechezea nafasi ya   kiungo ‘Frank Domayo’ amesaini mkataba wa miaka miwili  wa kuchezea kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara,  baada ya mkataba wake wa kuichezea Yanga kumalizika.

Usajili huo unakuja kufuatia mapendekezo ya kocha wa Azam JMO. ”Ili kuimarisha sehemu ya kiungo kama alivyopendekeza kocha mkuu JMO, AzamFC imemsajili Frank Domayo baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, tunaamini ushirikiano wa Domayo, Sureboy, Bolou, Himid, Brison na Mudathir utaifanya Azam FC iendelee kutakata. karibu Frank Chumvi Domayo Azam FC.Alisema Jemedari ambaye ni meneja na msemaji wa Azam Fc

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s