RONALDO NA RAMOS WAIPELEKA MADRID FAINALI UEFA, WAILOWESHA GOLI 0 – 4 BAYERN MUNICH

Sergio Ramos

Mlinda Mlango wa madrid Sergio Ramos akishangilia goli alilofunga dhidi ya Bayern Munich

Bayern Munich imeshindwa kulitetea taji lake baada ya kukubali kipigo cha bao 0 – 4  katika mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Real madrid  ya Hispania uliochezwa kwenye uwanja wa Bayern  ‘Allianz Arena’ usiku wa leo.

Ronaldo na Belle

Straika wa Madrid Cristiano Ronaldo akipongezwa na mchezaji mwenzake Gareth Bale baada ya kufunga goli.

Tofauti na matarajio ya watu wengi  waliokuwa na mtazamo tofauti huku wengi wao wakiipa nafasi kubwa Bayern kuibuka na ushindi hasa ikizingatiwa iko nyumbani lakini haikuwa hivyo na badala yake Madrid iliweza kuendeleza wimbi lake la ushindi na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ambapo atamsubiria mshindi atakayepatikana hapo kesho kati ya Chelsea au Atletico Madrid .

Pep Guardiola

Kocha wa Bayern Pep Guardiola akiwa haamini kilichotokea mbele ya macho yake

Magoli ya Madrid yalifungwa kwa ustadi   kupitia mpachika mabao wao Cristiano Ronaldo aliyetikisa mara mbili nyavu za Bayern  pamoja na mlinda mlango Sergio Ramos aliyetupia goli mbili zilizoiwezesha Timu yao kusonga mbele huku ikiwa na jumla ya magoli 5 kwa bila na kufuzu hatua ya Fainali ya michuano hiyo.

Carlo AncelottiKocha anayekinoa kikosi cha Real Madrid Carlo Ancelotti akishangilia kufuatia viajna wake kuibika na ushindi wa nguvu.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ambao utapigwa hiyo kesho nchini  Uingereza ambapo Chelsea watakuwa mbele ya mashabiki wao wa nyumbani wakijaribu kuvuka kizingiti kizito cha Atletico Madrid kuelekea Fainali.

Tazama Video ya magoli hapo chini

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s