AJALI : BASI LA SUMRY LAGONGA NA KUCHINJA WATU 19 MKOANI SINGIDA

 

sUMRY sINGIDA AJALI

Pichani ni Basi mali ya kampuni ya Sumry lenye namba za usajili T 799 BET baada ya kutokea kwa ajali.

Watu 19 wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Singida kufuatia ajali mbaya iliyohusisha basi mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likitokea mkoani Kigoma kwenda   jijini Dar es salaam  kuacha njia na kuvamia watu hao waliokuwa wakimtoa mtembea kwa miguu aliyefariki Dunia kwa kugongwa na lori mnamo majira ya saa moja na nusu usiku.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Geofrey kamwela amesema ajali hiyo mbaya  iliyotokea katika kijiji cha Utao wilayani Ikungwi, kilianza kwa lori kumgonga mtembea kwa miguu  na kufariki papo hapo, aliendelea kwa kusema wakati wananchi wakifanya utaratibu wa kuitoa maiti hiyo na kuiweka kwenye gari la polisi ndipo likapita basi la Sumry lenye usajili wa namba T 799 BET na ghafla likatoka nje ya barabara na kuwagonga watu waliokuwa wamefika eneo hilo na kuwakanyaga na kusababisha vifo vya watu hao.

aJALI YA SUMRY sINGIDA

Gari la polisi likiwa limebeba maiti za watu waliogongwa na basi la Sumry

Basi hilo lilokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Paul Njiro mkazi wa Dar es salaam, aliwagonga watu kadhaa waliokuwa kando ya barabara hiyo na kusababisha vifo vya watu 18 wakiwemo  askari polisi wa wanne kutoka katika kikosi cha FFU wa mjini Singida. Alisema kamanda huyo.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Singida Dr.Mussa Kimara amesema awali walipokea maiti 14 na zingine 5 zilikuwa katika hospitali ya misheni ya Puma  na majeruhi wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida wamepatiwa matibabu na wengine sita wanapatiwa katika hospitali ya misheni ya malikia wa ulimwengu ya Puma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema waliona gari la polisi likiwa barabarani  na walipotaka kulipita upande wa kulia wakaona kuna gari lingine linakuja  ndipo dereva wa basi hilo alipoamua kulipitisha basi hilo upande wa kushoto na kuwapitia watu ambao walikuwa nje ya barabara  na mara baada ya ajali hiyo dereva wa basi hilo alikwenda mpaka eneo moja linaloitwa Ikungi ambapo aliliacha gari na kutokomea kusipojulikana.

Singida 4 Singida Miili ya watu waliopoteza maisha ikiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida Singida3Singida2Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika eneo la hospitali hiyo ili kuweza kuitambua miili ndugu zao waliopteza maisha.

 

 

 

Advertisements

One thought on “AJALI : BASI LA SUMRY LAGONGA NA KUCHINJA WATU 19 MKOANI SINGIDA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s