NBA YAMFUNGIA MAISHA MMILIKI WA CLIPPERS ‘DONALD STERLING’ NA FAINI YA DOLA MILIONI 2.5

Chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani  ‘NBA’  kimemfungia maisha mmiliki wa Timu ya Los Angels Clippers ‘Donald Sterling’ mwenye umri wa miaka  80  kufuatia agizo lililotolewa na kamishna wa ligi hiyo  ‘Adam Silver’ sambamba na faini ya dola za kimarekani milioni 2.5 ambazo ni sawa na Tsh bilioni

Adhabu hiyo inamfanya Sterling  kutotakiwa kwenda kwenye mechi yoyote ya Clippers, kutohudhuria mazoezi  pamoja na kutofanya maamuzi yoyote ndani ya timu yake hiyo.

Baada ya uchunguzi kukamilika,  Donald alikubali  sauti iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya kwake wakati wa mazungumzo na kimada wake V.Stiviano ambaye alipigwa biti la kutopiga  picha na watu weusi au kuongozana nao katika mechi za Clippers.

Matamshi ya mmiliki huyo  yalionekana kuwachukiza na  kuwakera mastaa wakubwa kama vile ‘Magic Johnson, Snoop Dogg, Jadakiss, Lil Wayne, Lebron James na wengine kibao hali iliyopelekea wengi wao kumtole uvivu na  kuponda pasi na kupepesa macho.

Licha ya Sterling kutilia ngumu kwa kutotaka kuiuza timu yake hiyo, Wadau mbalimbali wenye mikwanja yao tayari wameshaanza kujitokeza kutaka kuichukua Timu hiyo jumla jumla huku asilimia kubwa ya watu wakimpendekeza   Magic Johnson.

Uamuzi uliotolewa na NBA umeonekana kuwafurahisha wadau na wapenzi wengi wa mchezo huo. Mbali na maamuzi hayo, taarifa zinasema kwamba hata muonekano wa logo na  Tovuti ya timu hiyo umebadiishwa na kuwa katika maandishi meupe yaliyo kwenye background nyeusi yaliyosomeka ‘WE ARE ONE LA CLIPPERS’ , slogani iliyoonekana kuungwa mkono na timu karibu zote zinazoshiriki ligi kuu ya NBA kwa kuanzisha Topiki kwenye mtandao wa Twitter iliyopewa jina la #WeAreOne ikiwa ni katika kuonyesha umoja na mshikamano  dhidi ya vitendo vya kibaguzi.

Clippers1

Brooklyn We Are One Chicago Bulls Cleveland  Dallas We Are On Denver Nuggets Detroit Golden & Indiana We Are On

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s