BEYONCE NDIYE MWANAMUZI MWEUSI ANAYEONGOZA KWA KULIPWA MKWANJA MREFU HIVI SASA

BeyonceBeyonce Knowlesa ambaye ni mke wa Rapa Jay Z’, ametajwa kuwa mwanamuziki wa kwanza mweusi anayeongoza kulipwa mkwanja mrefu kuwahi kutokea, huku akivunjilia mbali rekodi zilizowahi kuwekwa na wakongwe kama vile Michael Jackson, Prince na Janet Jackson baada ya  mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia ziara yake ya muziki iliyopewa jina la ‘The Mrs.Carter Show” World Tour .

Kwa mujibu wa jarida la Billiboard lilisema kwamba, Beyonce ameweza kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni 212 katika kipindi cha mwaka mzima alichokuwa akizunguka kufanya ziara zake za kimuziki  katika jumla ya miji 126 Duniani.

Bey & Jigga

Awali hitmaker huyo wa Drunk in Love alifanya ziara ya muziki katika bara la Ulaya iliyoanza mwezi Februari na kumalizika mwezi machi ambapo alifanikiwa kuzunguka katika miji ipatayo 25, na kumfanya aweke kibindoni   dola za kimarekani milioni 41.1 huku ngoma kama vile Drunk in Love na XO zinazopatika kwenye albamu yake ya tano ya Beyonce zikiendelea kumpandisha chati kutokana na kupendwa zaidi na  mashabiki wake.

Tayari Beyonce ameshatangaza Ziara mpya ya muziki iliyopewa jina la ‘On The Run’ atayofanya na mumewe Rapa jay Z katika miji mikubwa 16 iliyopo Marekani na Canada katika kipindi cha majira ya joto, itakayoanza Juni 25 na kumalizika Agosti 05 mwaka huu katika uwanja maarufu wa AT&T Park  uliopo katika mji wa San francisco.

Unaweza pia ukatazama hapo chini Tarehe pamoja na orodha ya miji watakayopita katika ziara yao ya muziki ya ‘On The Run’.

6/25 Miami, FL  – Sun Life Stadium 
6/28 Cincinnati, OH  – Great American Ballpark 
7/1 Foxborough, MA  – Gillette Stadium 
7/5 Philadelphia, PA  – Citizen’s Bank Park 
7/7 Baltimore, MD  – M & T Bank Stadium 
7/9 Toronto, ON  – Rogers Centre 8
7/11 East Rutherford, NJ  – MetLife Stadium 
7/15 Atlanta, GA  – Georgia Dome 
7/18 Houston, TX  – Minute Maid Park 
7/20 New Orleans, LA  – Mercedes-Benz Superdome 
7/22 Dallas, TX  – AT&T Stadium 
7/24 Chicago, IL  – Soldier Field 
7/27 Winnipeg, MB  – Investor Group Field 
7/30 Seattle, WA  – Safeco Field 
8/2 Los Angeles, CA  – Rose Bowl 
8/5 San Francisco, CA  – AT&T Park

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s