DANI ALVES AMZODOA SHABIKI ALIYEMRUSHIA NDIZI UWANJANI, WACHEZAJI NA MASHABIKI WALA NDIZI KUMUUNGA MKONO.

Dani Alves

Beki wa Barcelona Dani Alves akiila ndizi  iliyorushiwa na shabiki wakati wa mchezo dhidi ya VillaReal

Licha ya Viongozi wa ngazi za  juu katika soka FIFA kukemea na kutishia kutoa adhabu kali kwa yule yoyote anayebainika kufanya vitendo vya ubaguzi.  Hali imekuwa tofauti kwa  mamia ya mashabiki wa soka na wachezaji maarufu Duniani kwa kuamua kuonyesha upendo wao wa dhati kwa mchezaji Dani Alves wa klabu ya Barcelona kwa kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wakiwa wanakula ndizi .

Hali hiyo inafuatia na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na shabiki wake mmoja aliyemtupia ndizi Alves alipokuwa katika uwanja wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Hispania ya La Liga kati ya Barcelona na VillaReal.   Hata hivyo Alves akaiokota  ndizi hiyo na kuitia mdomo, kitendo kilichowagusa mashabiki wengi na wachezaji wengine wakubwa Duniani wakisema kuwa ni kitendo cha kijasiri cha kukabiliana na watu wanaoendeleza vitendo vya kibaguzi.

Alves' girlfriend Thaissa Carvalho

Mchumba wa Alves ‘ Thaissa Carvalho’ akila ndizi na mashabiki wakereketwa ikiwa ni ishara ya kumzodoa shabiki aliyemfanyia kitendo cha kibaguzi laaziz wake

Baadhi ya wachezaji hao walioweka picha zao katika mtandao wakionyesha wanakula ndizi ni pamoja na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, Mario Balotelli, Luis Suarez wa Liverpool, Oscar, David Luis na William  wote wa klabu ya Chelsea.  Mbali na watu hao, Rais wa Brazil ameandika kupitia akaunti yake ya Twitter ya kwamba mchezaji huyo ameonyesha ujasiri mkubwa  na kumzodoa shabiki aliyetupa ndizi uwanjani akidhani kuwa mchezaji huyo atakasirika.

Hata hivyo shabiki huyo amejikuta akikumbana na adhabu toka kwa uongozi wa klabu yake ya Villa Real ya kufungiwa kutoingia uwanjani katika mecho zote za nyumbani na klabu hiyo mpaka maisha yake yote. Kwa upande wa rais wa FIFA Sepp Blater ameendelea kukemea matukio hayo ya ubaguzi, akisema ni vibaya kwa vitendo hivyo kuendelea katika karne hii.

Mario BalotelliMario Balotelli hakuwa nyuma katika kumuunga mkono   Dani Alves.

Mousa Dembele and Nacer ChadliPichani ni wachezaji wa Fulham,  Mousa Dembele and Nacer Chadli

NeymarNeymar nae alikuwa bege kwa bega na Alves

Oscar, David Luiz and WillianWachezaji wa Chelsea Oscar, David Luiz and Willian

Philippe Coutinho and Luis SuarezMchezaji wa Liverpool Luis Suarez na Philippe Coutinho

Singida Ajali ya SumrySergio Aguero and Marta

talian Primer Minister Matteo Renzi and Italy coach Cesare PrandelliWaziri mkuu wa Italia(Wa kwanza kushoto) Matteo Renzi  na Kocha wa timu ya Taifa ya Italia Cesare Prandelli wakimuunga mkono Alves kwa kitendo cha ubaguzi alichofanyiwa.

Tazama video ya jinsi Tukio lilivyokuwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s