SNOOP DOGG, LIL WAYNE, SHAQ NA MAGIC JOHSON WACHUKIZWA NA KAULI YA KIBAGUZI ILIYOTOLEWA NA MMILIKI WA CLIPPERS

Mmiliki wa Clippers Donald Sterling akiwa na mpenzi wake aliyekaa kushoto kwake

Mmiliki wa Clippers Donald Sterling akiwa na mpenzi wake Stiviano aliyekaa kushoto kwake

Mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angels Clippers ‘Donald Sterling’ amejikuta akiambulia matusi na kujishushia heshima yake kutoka kwa wamarekani weusi baada ya kauli za kibaguzi alizokuwa akimtolea mpenzi wake Stiviano wakati wa mazungumzo yao kudakwa kwenye  kinasa sauti hali iliyopelekea mastaa wakubwa kama vile Snoop Dogg, Lil Wayne, French Montanna, Kobe brayant, Shaq, Lebron na mchezaji wa zamani wa timu ya lakers Magic Johnson kukasirishwa na kuamua kumtolea uvivu.

Licha ya timu yake kujaa wahezaji wengi weusi waliopata kutwaa mataji mbalimbali makubwa, taarifa zinasema kwamba Sterling hakutaka kabisa mpenzi wake apige picha na mtu  mweusi ikiwemo na sharti la kutomleta rafiki yake yeyote mweusi katika mechi za Clippers.

”Ni aibu kwa Donald Sterling kuonyesha ubaguzi kwa watu wenye asili ya afrika. Timu yake ina wachezaji wengi weusi ambao wanafanya kazi ya kumletea ubingwa na kuongeza idadi kubwa ya mashabiki.  alisema Maagic Johnson.

Mtandao wa TMZ uliweza kupata walizungumza baadhi ya mastaa nyota wenye asili ya Afrika akiwemo Lebron, Shaq, Kobe, Snoop, Lil Wayne na Montana  kuhusiana na kauli tata alizotoa Sterling…. Sikiliza hapo chini  walichosema ikiwemo na mazungumzo yaliyosababisha tafrani.

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s