GIGGS AANZA VIZURI NA MAN UNITED KWA KUITANDIKA BAO 4 – 0 NORWICH, EVERTON YACHEZEA BAO 2 – 0 NA SOUTHAMPTON

Giggs

Kocha wa muda wa Manchester United ‘Ryan Giggs’ ameuanza vizuri mchezo wake wa kwanza tangu akabidhiwe madaraka ya kukinoa kikosi hicho kwa muda  baada ya kuichezeshea kipigo kikali Norwich City hapo jana katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa  Old Trafford ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu kufukuzwa kwa  kocha David Moyes.Wayne Rooney1Magoli ya United yalifungwa na mshambuliaji Muingereza au unaweza kumuita baba wa watoto wawili Wayne Rooney mnamo dakika ya 41 kwa mkwaju mkali wa mpira wa adhabu na lingine akifunga dakika ya 48′ kabla Juan mata kukamilisha karamu  ya magoli kwa kupachika  goli mbili wavuni na kuipa ushindi  United wa   wa goli 4 kwa Nunge.

 

Mchezo mwingine uliochezwa hapo jana ulikuwa ni kati ya Everton waliokubali kuchezea kipigo cha bao mbili kwa bila toka kwa vijana wa Saint Mary’s,  klabu ya Southampton licha ya magoli yote kuwa ya kujifunga kwa uzembe uliofanywa na  Antolin Alcaraz na Seamus Coleman.

Fergie

Kwa mujibu wa ligi kuu ya England, hivi sasa Southampton inashikilia nafasi ya 8 ikiwa na pointi 52 wakati Everton ikikamata nafasi ya 5 ikiwa na   pointi 69 huku kukiwa kumesalia michezo kadhaa kuweza kufungwa kwa pazia la ligi kuu.

Mata

Unaweza ukatazama video za magoli hapo chini ya mchezo kati ya Manchester United na Norwich pamoja na Southampton na Everton

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s