ZAMBIA YAOMBOLEZA KIFO CHA MTANGAZAJI GWIJI WA SOKA ‘DENNIS LIWEWE’ KWA SIKU TATU

Dennis Liwewe - Larrybway91

Marehemu Dennis Liwewe

Jamii ya wanamichezo hususani wapenzi wa mpira wa miguu nchini Zambia inaomboleza kifo cha mtangazaji  gwiji wa soka mzee Dennis Liwewe ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa habari za michezo wa BBC idhaa ya kiingereza katika kipindi cha Focus on Africa. Serikali ya Zambia imetangaza siku tatu za maombolezo  huku bendera kupepea nusu mlingoti  kwa heshima ya nguli huyo wa utangazaji.

Utangazaji wa Liwewe ulikuwa ni wa  mzuka na hamasa kwa soka la Zambia, hali iliyompelekea asafiri  zaidi ya mara 96 katika nchi 42 akiwa na timu ya Taifa ya soka ya Zambia ijulikanayo kama Chipolopolo.

Mzee Dennis Liwewe ambaye alifariki hapo juzi akiwa na umri wa 78, alifanya kazi ya utangazaji wa soka kwa zaidi ya miaka 50 kabla ya kustaafu mwaka 1993  kwa ushauri wa madaktari kufuatia mshituko wa moyo alioupata  kufuatia ajali ya ndege iliyouwa wachezaji wote wa timu ya soka ya taifa ya zambia Aprili 28 mwaka huo ambapo yeye alinusurika ajali hiyo baada ya kuchelewa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea nchini Senegal.

Utangazaji wake wenye hamasa na uzalendo mkubwa ulimfanya atambulike na kuheshimiwa nchini zambia ambapo alichukuliwa kama mmoja wa watu maarufu  wenye ushawishi mkubwa .

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s