CHIDY BENZ AMPASUA ZILIPENDWA WAKE, ASHONWA NYUZI 18 MDOMONI, ATIWA MBARONI

Mwanaisha_1

Rapa mtukutu wa kundi La Familia lenye maskani yake Ilala  ‘Chidy Benz alijikuta  akiimalizia sikukuu yake ya Pasaka nyuma ya nondo baada ya kumtembezea kichapo cha mbwa mwizi mpenzi wake wa zamani aliyetajwa kwa jina moja la Mwanaisha kwa kile kilidaiwa kuwa ni kumchoresha mbele ya mpenzi wake mpya.

Tukio hilo lililojiri katika Bar moja iliyopo maeneo ya flati za Ilala mahala ambapo amekulia staa huyo. Chidi Benz alidai kwamba, siku ya tukio alikuwa akirudi nyumbani kwao huku akiwa ameongozana na mchuchu wake, ndipo ghafla akasikia sauti ya Mwanaisha aliyekuwa akisema  ”Naona upo na mama watoto” huku akirudia neno hilo takribani mara nne.

Baada ya kugundua sauti ile ilikuwa ni ya zilipendwa wake,  ndipo varangati lilipoanza hali iliyopelekea rapa huyo kumtembezea kichapo heavy, kilichopelekea bi mdada huyo kupasuka vibaya maeneo ya mdomo na kujikuta akishonwa nyuzi 18 na kisha kumfungulia kesi iliyopewa RB/1569/2014 na hatimaye kuweza kufanikisha zoezi la kumkamata rapa huyo,  licha ya hapo baadae kutolewa kwa dhamana ya shilingi laki moja hali iliyopelekea ndugu wa Mwanaisha kulalama   huku wakidai ndugu yao amekuwa akizimia   mara kwa mara.

Mwanaisha1Mwanaisha

Picha na Video kwa hisani ya Global Publishers

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s