Kwa wale wafuatiliaji wa masuala ya matukio makubwa yaliyowahi kuikumba Afrika Mashariki, bila shaka utakuwa unamfahamu mtangazaji mpekuzi wa makala maalum ya Jicho Pevu ‘Mohammed Ali’ wa kituo cha KTN cha nchini Kenya.
Mojawapo ya vitu vilivyowahi kumwongezea umaarufu mtangazaji huyo ni pamoja na sakata la suvamizi wa jengo la Westgate septemba 23 mwaka jana ikiwemo na kifo kilichozua utata cha profesa George Saitotit na hivyo kumfanya awe gumzo ndani na nje ya bara la Afrika.
Mbali na kazi ya uandishi wa habari, Mohammed Ali pia ni mpenzi wa magari, akiwa na anamiliki jumla ya magari matano ikiwemo Toyota Carib, Toyota Mark X, Mitsubishi Gallant, Toyota Kluger, Toyota VX. na jipya aina ya BMW convertible.
Hapa akiwa na BMW yake Convertible
Mohammed Ali akiwa amepozi katika mkoko wake mwingine aina ya VX