AFISA MKUU WA FACEBOOK ‘SHERYL SANDBERG’ AWAHIMIZA WANAWAKE KUSHIKILIA NAFASI MUHIMU KATIKA BIASHARA

Sheryl Sandberg na Mark Zuckerberg

Muanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg akiwa ameketi na Sheryl Sandberg

Afisa mkuu wa mipango wa Facebook, mwanamama Sheryl Sandberg amewahimiza wanawake wenzake Duniani kote kuacha kubweteka na kuwa tegemezi bali kutakiwa kushikilia nafasi muhimu katika biashara.

”Ukiwa unatafakari kufanya kitu,  jiulize nini unachoweza kufanya, ikiwa hauna uwoga na basi ukifanye” alisema Sandberg wakati alipofanyiwa mahojiano na kituo cha utangazaji cha BBC.

Sherly Sandberg ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika kampuni ya Facebook tangu mwaka  2012, huku mwaka jana akiwa ameandika kitabu ‘Lean In’ na katika kitabu hicho anawashauri wanawake waanze kushikilia vyeo katika meza za maamuzi.

Alikuwa anawaambia ni jinsi gani wanavyoweza kupiga hatua za nafasi zao za kazi na kusema kuwa ni muhimu sana kwa wanawake ambao nusu   ya idadi ya watu wote waanze kushikilia vyeo katika meza za maamuzi, lakini bado alisema hatujafika hapo.

Alisema Wanawake wanaweza kuwa viongozi muhimu sana katika biashara, Serikali na pamoja na kuwa wajasiriamali.

”Dunia inashuhudia mageuzi makubwa ya kiteknolojia ambayo yanahusisha simu ya rununu na facebook ipo katikati ya mageuzi hayo” alisema Sandberg alipokuwa akizungumzia changamoto zinazoikumba mtandao wa Facebook

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s