MLINDA MLANGO WA AC BONGOVILLE ‘SYLVAIN AZOUGOUI’ AFARIKI DUNIA

Mlinda mlango wa  klabu ya AC Bongoville  ‘Sylvain Azougoui’  amefariki dunia mara baada ya kuumia kichwani wakati wa mchezo wa ligi kuu huko Gabon.

azougouii

Sylvain Azougoui

Kipa huyo Raia wa Togo mwenye umri wa miaka 30  alifikwa na umauti akiwa njiani kukimbizwa hospitalini  baada ya kutokea kwa tukio hilo, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Centre Mberi Sportif.

Sylvain Azougoui

Taarifa zimesema Azougoui alikumbana na mkasa huo wakati akizuia moja ya shambulizi  langoni mwake lakini kwa bahati mbaya aligongana katika eneo la kichwa na mshambuliaji wa timu pinzani, hali iliyopelekea kufikwa na umauti.

Familia ya mpira wa miguu ya Gabon, imetoa pole kwa familia ya marehemu ambayo ipo Togo pamoja na klabu yake kwa ujumla bila kusahahu shirikisho la soka la Togo  ambapo goli kipa huyo anatokea.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s