MBUNGE MWINGINE WA SOMALIA AFARIKI DUNIA LEO KWA KUSHAMBULIWA NA WANAMGAMBO

Gari la mbunge

Katika picha ni gari ambalo lilitegwa bomu lilopelekea kuchukua uhai wa mbunge wa Somalia hapo jana(Jumatatu)

Mbunge wa Somalia Abdiaziz Isak ameuwawa na wanamgambo wa Al – Shabab hii leo, yakiwa ni mauaji ya pili ya aina hiyo kufanywa katika kipindi cha masaa 24.

Afisa wa Polisi Mohamed Dalane amesema mbunge huyo amepigwa risasi mara kadhaa na kufa papohapo karibu kabisa na mahali ambapo mbunge mwingine aliuwawa katika kitongoji cha Madina  katika mji mkuu Mogadishu.

Jana mbunge aliuwawa  na mwingine kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa  kwenye gari ambalo linadaiwa kufanywa na kundi la Al-Shabab  lenye mafungamano na  kikundi cha Al Qaeda.

Kundi la Al-Shabab limetishia kuwauwa wabunge wote katika serikali ya Somalia  inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Mauaji ya leo yamefanyika huku serikali ikikutana kwa siku ya mwisho ya mkutano kuhusu usalama ikitumai kukabiliana na mashambulizi ya Al Shabab.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s