DAVID MOYES AFUNGASHIWA VIRAGO, GIGGS KUKAIMU NAFASI YAKE KWA MUDA

David Moyes

David Moyes

Bodi ya Manchester United imethibitisha rasmi kusitisha mkataba wake na kocha David Moyes aliyekuwa akikinoa kikosi hicho cha mashetani wekundu, huku kipigo cha juzi kutoka kwa Everton  katika dimba la Goodson park cha mabao mawili kikitajwa kuwa mojawapo ya sababu kubwa zilizochangia kupigwa chini kwa kocha huyo na kufanya kufifia kwa  ndoto za vijana hao wa Glazer kucheza klabu bingwa barani ulaya hapo mwakani.

Huku kampuni kama vile ya NIKE inayowafadhili vifaa vya michezo ikionekana kama kutaka kukimbia kutokana na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa timu kwa hivi sasa.

Nafasi ya Moyes imetajwa kukaimiwa na mchezaji nguli wa timu iyo, Ryan Giggs mpaka pale atakapopatikana kocha mpya.

Awali Moyes alichaguliwa kuchukua nafasi ya umeneja  na kocha wa zamani wa United, Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa ameshikilia hiyo nafasi kwa takribani muda wa miongo miwili  na nusu, huku akiamini kuwa ndiye kocha ambaye angeweza kuleta mabadiliko katika timu hiyo sambamba na kuwa na historia ya kuka na timu kwa muda mrefu.

David Moyes alipewa mkataba wa miaka sita wa kuinoa Manchester United akiwa tayari ameshaongoza jumla ya michezo 51 tangu ajiunge na kikosi hicho cha Old Trafford.

Katika mechi 51 ambazo tayari amezisimamia, ameweza kushinda mechi 27, amekwenda sare mechi 9 na kufungwa mechi 15 na hivyo kufanya asilimia ya ushindi kuwa 52.94, hali inayoonyesha matokeo mabaya katika historia ya Manchester.

Mpaka sasa bado hakujakuwepo na taarifa za hatima ya kocha huyo kama ataendelea kulipwa mshahara wake ndani ya kipindi cha miaka sita iliyobakia  kama jinsi inavyokuwa kwa makocha wengine  pindi wanapokuwa wamefukuwa kwenye vilabu walivyokuwa wakifundisha.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s