BASI LAGONGA NYUMBA NA KUCHINJA WATU 11 PAPOHAPO

Luhuye BasiBasi la Luhuye baada ya kuvamia nyumba.

Basi_La_LuhuyeBasi la Luhuye

Watu 11 wamepoteza maisha  papohapo na mwingine mmoja kufariki  dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali  ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.

Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi  katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Itwilima kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa  ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.

 Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali  hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo.

 Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na miili 11 ya marehemu.

 Amesema kati ya majeruhi hao 25  hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.  Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Chanzo : ITV

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s