KIBARUA CHA KOCHA WA MAN UTD ‘DAVID MOYES’ HATARINI KUOTA NYASI MUDA WOWOTE

Moyes David

David Moyes

Bodi ya klabu ya Manchester United wakati wowote kuanzia sasa itafanya maamuzi magumu ya kumfukuza kazi kocha wake David Moyes(50) na hiyo ni kutokana na matokeo mabaya kuwahi kukikumba kikosi hicho kinachoshiriki ligi kuu ya kandanda ya England (EPL).

Hata hivyo uongozi wa Manchester United umegoma kuzungumzia chochote kile kuhusiana na taarifa za David Moyes kupokonywa kibarua chake cha ukocha mkuu wa kikosi hicho.

Baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba uongozi uko mbioni kusitisha mkataba  wa miaka sita aliopewa meneja huyo kufuatia matokeo mabovu  wanayoendelea kuyapata.

Ikumbukwe kuwa David Moyes aliteuliwa na Sir Alex Ferguson kuruthi nafasi yake ya umeneja wa kikosi hicho  wakati alipoamua kujiweka kando  na kustaafu kibarua hicho cha takribani miaka ishirini na sita.

Kwa sasa Manchester United inakamata nafasi ya saba huku wakiwa wamesaliwa na michezo  minne kukamilisha ligi lakini wamejikuta wakiwa kwenye wakati mgumu huku wakiandika historia ya kuwa na alama chache sambamba na matokeo mabovu kuliko  misimu iliyopita.

Mashabiki wa mashetani wekundu jana kwa mara nyingine tena walikutana dhoruba  ya kupokea dozi  ya mabao mawili kwa nunge kutoka kwa vijana wa Goodson Park ‘Everton’  iliyokuwa timu ya zamani ya kocha David Moyes.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s