TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI LA PSQUARE, PETER NA PAUL WADAIWA KURUSHIANA MAKONDE, KISA???

PsquareUle msemo usemao Adui anaweza kuwa rafiki na rafiki akawa adui umejidhihirisha wazi wazi kupitia familia ya muziki kutoka nchini Nigeria ‘Psquare’ inayoundwa na mapacha wawili waliozaliwa tumbo moja,  Peter na Paul Okoye kudaiwa kuingia katika mgogoro uliopelekea kuzichapa kavukavu  walipokuwa kwenye mazoezi  jumatano iliyopita  hali iliyopelekea wacheza shoo wao kuamulia na kufanikiwa kuwatenganisha.

Kwa mujibu wa taarifa zinadai kwamba,  kumekuwa na mvutano wa familia ya Okoye huku mke wa Peter aitwae Lola Omotayo akitajwa  kuwa ndio chanzo cha mapacha hao kuingia kwenye ugomvi hali iliyopelekea kuzuka kwa tetesi kuwa huenda ukawa ndio mwanzo wa kusambaratika kwa kundi hilo lililodumu na kupata mafanikio makubwa kimataifa kupitia sanaa ya muziki kwa kipindi cha takribani miaka 10.

Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa meneja wa kundi hilo, Jude Okoye’ ambaye ni kaka mkubwa wa Psquare  na mke wa Peter kudaiwa  kutopikia chungu kimoja, hali iliyompelekea kutohudhuria sherehe yao ya kimila  iliyofungwa mwaka jana jijini Lagos, Nigeria.

Peter na Paul waliopanga  kufanya sherehe jijini Dubai,  walijikuta wakifikia hatua ya kubishana huku upande mmoja ukitaka kaka yao ahudhurie harusi hiyo licha ya kuwepo kwa vijimaneno kutoka kwa mke wa Peter ‘Lala’  kutotaka Jude kuhudhuria sherehe yao.

”After over 10yrs of hard work, it’s over. Am done”. ilikuwa ni moja ya ujumbe alioandika Jude Okoye kupitia ukurasa wake wa Twitter.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s